Saturday , 7th Nov , 2015

Mwenyekiti wa Jumuiko la Maliasili nchini (TNRF) Dr. Suma Kaare amemtaka Rais John Pombe Magufuli kudhibiti upotevu wa maliasili za wanyama pori na misitu uliokithiri katika maeneo mengi nchini ili kunusuru uhai wa maliasili.

Dr. Suma Kaare Mwenyekiti wa Jumuiko la Maliasili nchini (TNRF)

Mwenyekiti wa Jumuiko la Maliasili nchini (TNRF) Dr. Suma Kaare amemtaka Rais John Pombe Magufuli kudhibiti upotevu wa maliasili za wanyama pori na misitu uliokithiri katika maeneo mengi nchini ili kunusuru uhai wa maliasili.

Suma Kaare amesema hayo katika mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili unaoendelea jijini Arusha, Kaare amesema kuwa jukwaa hilo litashirikiana na Rais huyo katika kuhakikisha kuwa maliasili zinalindwa na kuwanufaisha watanzania kwa kiwango stahiki.

Mratibu wa masuala ya misitu katika shirika la uhifadhi wa maliasili na mazingira (WWF), Isaac Malungu amesema kuwa asilimia 90% ya nishati inayotumika nchini inatokana na kuni pamoja na mkaa hali ambayo inaathiri misitu na kutishia uhai wa maliasili nchini hivyo ameitaka serikali ihimize matumizi ya nishati mbadala ili kunusuru mazingira yanaoharibiwa kila kukicha.

Mkurugenzi wa shirika la AWF John Salehe amesema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi amesababisha hali ya ukame inayowaathiriwanyama pamoja na mimea hivyo kuathiri uhifadhi kwa ujumla.

Juhudi zaidi zinapaswa kuchukuliwa ili kulinda maliasili ikiwemo upandaji wa miti pamoja na kutunza misitu ili kurejesha uoto wa asili uliopotea.