Thursday , 28th Aug , 2014

Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amesema kamati ya ulinzi na usalama haip tayari kuona watu wake wanapoteza maisha na kuwataka wakazi wa Arusha hususani wanawake kuwa watulivu kwa kuwa mamlaka zinalifanyia kazi suala la mauaji ya wanawake.

Wito wa mkuu wa mkoa umekuja huku kukiwa na taarifa za wanawake kukutana leo katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Arusha kupinga mauwaji ambayo mpaka sasa jeshi la polisi limedhibitisha watu watu wawili kuuwawa na mwingine mmoja kujeruhiwa.

Akiongea na waandishi wa habari jana kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amesema idadi ya watuhumiwa kuhusiana na matukio hayo ya upigaji risasi wanawake jijini Arusha imefika nane baada ya jana mtuhumiwa Adamu Juma ambae tayari amekiri kushiriki katika matukio kadhaa kukamatwa.

Kauli ya mkuu wa mkoa Mulongo imekuja siku moja baada ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas kusema kuwa jeshi hilo linamshikilia mtuhumiwa Adam Mussa mwenye umuri wa miaka 30, mkazi wa Majengo Jijini Arusha, kwa kukamatwa na bastola mbili zikiwa na risasi, ambaye anatuhimwa kuhusika na matukio ya kuwapiga risasi wanawake mjini Arusha.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo , Kamanda Liberatus Sabas amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa Agosti 26 mwaka huu, majira ya usiku, nyumbani kwake Majengo Juu.

Kamanda Sabas amesema baada ya kumkamata mtuhumiwa na kumhoji ambapo alikiri kuhusika katika matukio yanayoendelea jijini Arusha ya upigaji wanawake risasi na moja kati ya silaha hizo iliibiwa ndani ya gari la mfanyabiashara Seleman Bakari Msuya mkazi wa Sombetini, baada ya watu wasiojulikana kuvunja kioo cha gari na kuichukua. Mtuhumiwa anatarakiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kumalizika.

Kamanda Sabas ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa siri za mtandao huo uliozuka ghafla mwezo Agosti mwaka huu na kujeruhi na kuua
wanawake wenye magari mjini Arusha, ambapo hadi sasa tayari watu nane wanashikiliwa kwa kuhusiana na matukio hayo.