
Mkazi wa jiji la Dar es Salaam akiwa katikati ya nyumba zilizozingirwa na mafuriko kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha
Madiwani hao wametoa wito huo leo jijini Dar es salaam wakati wa kikao cha pamoja kati yao na Meya wa manispaa ya kinondoni Mh. Yusuph Mwenda pamoja na mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni Bw. Musa Nate kikao ambacho kilikuwa na lengo la kujadili athari za mafuriko zinazojitokeza kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Hata hivyo kutokana na malalamiko mengi ya madiwani hao Meya wa Kinondoni Yusuph Mwenda ameahidi kutoa fungu la fedha kwa ajili ya kukarabati miundo mbinu iliyoharibika kutokana na mvua hizo huku akiwataka wananchi wa manispaa hiyo waishio katika maeneo hatarishi kuondoka mara moja kutokana na mvua hizi kuendelea hadi mwezi wa tano mwaka huu....NEWS CLIP 4PM SWA UG..........