
Picha ya tukio wakati ngumi zikiendelea ukumbini
Ngumi hizo zilizohusisha Madiwani wa pande zote mbili zimetokea baada kuwepo kwa sintofahamu wakati wa kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo jioni ya leo.
Hata hivyo msimamizi wa uchaguzi huo Jabir Makame, aliendelea kwa kumtangaza Omar Kumbilamoto kama mshindi wa nafasi hiyo.
Omar Kumbilamoto (CCM), amepata kura 27 akifuatiwa na Mgombea Adam Rajabu (CUF) aliyepata kura 25 huku Mgombea Patrick Assenga (CHADEMA) akikosa kura hata 1.
Matokeo hayo yalizua utata ndipo madiwani wa CHADEMA wakaanza kurushiana maneno na wale wa CCM kabla ya kufikia hatua ya kutwangana ngumi ambazo ziliamuliwa na askari na hali ikarejea kuwa shwari.
Kumbilamoto ambaye ni diwani wa Vingunguti ndiye alikuwa Naibu Meya kupitia CHADEMA kabla ya hivi karibuni kujiuzulu udiwani na kuhamia CCM ambako ameshinda kwenye uchaguzi mdogo wa Septemba 16, 2018 na leo ametetea nafasi yake hiyo ya Naibu Meya.