Sunday , 13th Jul , 2014

Baadhi ya maaskofu na wachungaji wa makanisa ya kipentekoste na Sabato nchini Tanzania wamejikuta wakiingia katika mjadala wa umri pamoja na nani anafaa kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao

Moja ya makanisa ya Kipentekoste

Baadhi ya maaskofu na wachungaji wa makanisa ya kipentekoste na Sabato nchini Tanzania wamejikuta wakiingia katika mjadala wa umri pamoja na nani anafaa kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao huku wakielezea namna kanisa linavyokerwa na vitendo vya ufujaji mali za umma unaofanywa na viongozi wasio waadilifu.

Katika mkutano wao na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, wachungaji hao wamesema kanisa linataka mgombea wa umri wowote kuanzia miaka thelathini ambayo kiimani ndiyo umri ambao Yesu Kristo alianza kuwatumikia wanadamu na kwamba busara na hekima havina uhusiano na umri.

Akiongea katika mkutano huo, Askofu mkuu wa kanisa la Jesus Power Miracle Church, Joachim Peter amesema kuna haja ya vijana kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za juu za uongozi kama ambavyo baadhi wameanza kuonyesha njia huku akionyesha namna nchi inavyoitaji vijana waadilifu kwa ajili ya kulisaidia taifa kukabiliana na changamoto za kiuongozi na maadili.