Friday , 25th Apr , 2014

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii nchini Tanzania Dkt. Seif Rashid, amesema kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa Tanzania Bara kimepungua kwa takriban asilimia 50 kutoka asilimia 18 mwaka 2008 hadi asilimia 10 mwaka 2012.

Picha ya mbu, mdudu anayeambukiza ugonjwa wa malaria

Dk Seif ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Malaria duniani inayoadhimishwa dunaini kote kuanzia leo.

Waziri Seif amesema kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa huo kumeenda sambamba na kupungua kwa vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano vinavyotokana na ugonjwa huo kutoka vifo 148 kwa kila watoto 100 waliozaliwa hai mwaka 1999 hadi vifo 54 mwaka 2013.