Friday , 28th Aug , 2015

Maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi yameongezeka katika mkoa wa Kigoma kutoka asilimia 1. 8 mwaka 2008 hadi asilimia 3.4 hivi sasa hali ambayo inahatarisha afya na kuongeza idadi ya vifo hasa kwa akinamama wakati wa kujifungua.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Lenard Subi

Takwimu hizo zimetolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Lenard Subi wakati wa ufunguzi wa ofisi ya shirika la kimataifa la world lung foundation, linalojishughulisha na uboreshaji afya ya mama na mtoto

Dkt. Subi amesema katika kukabiliana na maambukizi mapya pamoja na utoaji wa elimu, wamezindua huduma za upimaji virusi vya ukimwi katika sehemu zote za huduma za afya ili kuwakinga watoto wanaozaliwa.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa shirika la World Lung Foundation nchini Dkt. Nguge Mwakatundu amesema lengo la shirika hilo ni kupunguza vifo vya akinamama kwa asilimia kubwa, sambamba na kuwezesha asilimia themanini ya akinamama kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma.