Monday , 12th Sep , 2016

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imepiga marufuku wananchi kuvamia mashamba ya wawekezaji wanayoyamiliki kihalali na kujihusisha na uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi mjini Ifakara Wilayani Kilombero mkoani Morogoro wakati akizungumza na viongozi wa serikali ya wilaya mkoa, madiwani na wananchi.

Mhe. Lukuvi amesema serikali itaendelea kuwalinda wawekezaji na wananchi wanaomiliki ardhi kihalali kwa ajili ya shughuli za uzalishaji wa mazao na kuhakikisha wawekezaji wenye hati kihalali wanaheshimiwa.

Amesema hakuna tatizo kwa mwekezaji kumiliki sehemu kubwa ya ardhi ili mradi awe anamiliki kihalali na afuate sheria ikiwemo uendelezaji wa mashamba hayo kulingana na hati miliki yao.