Wednesday , 29th Jul , 2015

Waziri mkuu wa Zamani, na aliekuwa Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa jana ametangaza rasmi kujitoa Chama Chama cha Mapinduzi na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kinachounda umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA.

Mh. Freeman Mbowe (kushoto) akimpongeza Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa mara baada ya kujiunga na CHADEMA.

Akiongea jana Jijini Dar es Salaam kwenye mkutano na Waandishi wa Habari Lowassa amesema amechukua uamuzi huo baada ya kutafakari kwa kina na kukubali kujiunga na CHADEMA, kwa lengo la kuungana na upinzani katika kuleta mabadiliko ya Kweli.

Aidha Lowassa alitoa sababu zilizomuondoa ndani ya chama chake kuwa ni pamoja na mezingwe,ukiukwaji wa maadili ya, uvunjaji wa Katiba ya Chama hicho pamoja na chuki za dhahiri dhidi yake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe wakati wa hotuba yake ya kumkaribisha amesema wanachama waatambue chama hicho ni cha wote na ni wajibu wake kujenga mshkamano kwa wote na chedema sio mahakama kwa hivyo haiweze kumuhukumu.

Wakizungumza kwa nyakati Tofauti Wenyeviti wa Umoja wa Katiba ya Wananchi Wamesema kuwa Wamempokea kwa mikono miwili Mh. Edward Lowassa na kuahidi kushirikiana nae katika kuleta mabadiliko ya kiasiasa nchini Tanzania.