Wednesday , 4th Jun , 2014

Upungufu wa Vitamini na Madini umetajwa kuwa moja wapo ya matatizo makubwa ya ki-lishe yanayopelekea kuathiri watoto na wanawake, ambapo upungufu wa madini chuma ukiathiri asilimia 59 ya watoto wadogo na asilimia 41 ya akina mama wajawazito.

Baadhi ya vyakula ambavyo ndio chanzo kikuu cha vitamini na madini kwa watoto na akina mama wajawazito.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Elifatio Towo na kueleza kuwa tatizo la upungufu wa Vitamini A linaathiri asilimia 33 ya watoto walio na umri chini ya miaka mitano na asilimia 37 ya wanawake waliokatika umri wa kuweza kubeba ujauzito.

Naye Mtaalamu wa lishe ya watoto wadogo na wachanga Bi. Neema Joshua ameelezea umuhimu wa mama mjazito kuzingatia lishe bora yenye vitamini na madini ili kuweza kupambana na matatizo hayo.

Tags: