Friday , 28th Jun , 2019

Mwanafunzi Idrisa Abdallah Nandepe (13) anayesoma Shule ya Msingi, Wilaya ya Liwale, Mkoa wa Lindi amenusulika kifo baada ya kutekwa na watu wasiojulikana alipokuwa akienda shuleni.

Akizungumzia tatizo hilo Idrisa anayesoma darasa la 7, amesema akiwa anaelekea shuleni, alikutana na watu watatu wenye jinsi ya kiume, asiowafahamu wakiwa wamesisima njiani na alipokuwa anawapita baada ya kuwasalimia walimzingira na kumshika na kumchomolea kisu wakimtaka asipige kelele na kumpeleka kichakani.

ameendelea baada ya kumfikisha kwenye kichaka hicho cha makaburi walimuweka chini ya ulinzi kwa masaa manne, akiwa amefungwa kamba kwenye mikono yake miwili huku mmoja wa watekaji hao akipiga simu kuwataka wapeleke Gari kwani tayari mzigo walioutaka umepatikana.

"Baada ya kunitaiti walinichomolea kisu na kuniambia nisipige kelele na kunipeleka kichakani, eneo la makaburini na kuniweka kwa masaa manne" Alisema Idrisa.

Idrisa alisema baada ya Gari ndogo yenye rangi ya Silver, bila kutaja namba kuwasili eneo lile mmoja wa watekaji hao alimshika bega kwa ajili ya kumpakia na kumpeleka asikokujuwa alifanikiwa kuwaporonyoka na kukimbilia nyumbani kwa dada yake aitwae Zuhura Abdallah Nandepe na kumuelezea mkasa uliomkuta.

Alisema baada ya kumpatia maelezo hayo alimueleza waende kituo cha Polisi Liwale mjini akatoe taarifa,jambo ambalo alilikubali na kulitekeleza mara moja.

"Hili gari tulishaliona mara nyingi likifika inafika eneo la Nyumbani kwetu, linakaa kwa muda kisha kuondoka,lakini hatukujua lengo lilikuwa kuniwinda mimi masikini"Alisema Idrisa.

Baba wa mwanafunzi huyo,Abdallah Nandepe,akizungumza na mwandishi wa Habari hizi alisema taarifa za kutekwa kwa kijana wake huyo alizipatia kupitia kwa motto wake mkubwa aitwar Mustafa Abdallah Nandepe na kuanza kufuatilia Kituo cha Polisi cha Liwale mjini.

Kamanda wa Polisi Mkoani Lindi, ACP Prodansiana Protas alipouliza kuhusiana na tukio hilo, amekiri kutokea na kueleza tayari askari wanaendelea kulitafuta gari na watekaji wanaohusika na kitendo hicho ili Sheria iweze kuchukuwa nafasi yake.