Dkt Besigye amefikishwa katika majengo ya mahakama mapema kabla ya saa tatu, muda wa kawaida wa kufunguliwa kwa mahakama, na akasomewa mashtaka.
Leo imekuwa mara ya pili kufikishwa mahakamani akikabiliwa na tuhuma hizo za uhaini ambapo awali alifikishwa mahakani kwa mara ya kwanza siku ya Ijumaa iliyopita katika mji wa Moroto, kwa madai ya kujiapisha mwenyewe kuwa Rais wa Uganda.
Aidha kiongozi huyo amejiwakilisha mwenyewe kortini na amesema kuwa hataki kuhusisha mawakili katika kesi hiyo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni Mosi ambapo Dkt. Kizza Besigye amerudishwa rumande.
Chanzo BBC




