Kauli ya serikali imetolewa bungeni na waziri viwanda biashara na uwekezaji Charles Mwijage wakati akijibu swali la mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari (Chadema).
Nassari ametaka kujua kwanini serikali imekuwa na ahadi zisizotekezeleka hususani kwa kiwanda cha general tyres ambacho kilikuwa kikitoa matairi bora kuliko mengine katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.
Akijibu swali hilo waziri mwijage amesema kinachofanyika sasa ni kubadili mitambo ya kiwanda hicho kwa kuwa iliyokuwepo imechakaa na baada ya muda mfupi kiwanda hicho kitaanza kazi ili kiweze kuajiri mamia ya vijana wengi.



