Saturday , 4th Jun , 2016

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa pamoja na wenye nyumba za kupangisha jijini Dar es Salaam kuhakikisha kuwa wanakuwa na picha za wapangishaji wanaopangisha katika nyumba zao kwasababu za usalama.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa pamoja na wenye nyumba za kupangisha jijini Dar es Salaam kuhakikisha kuwa wanakuwa na picha za wapangishaji wanaopangisha katika nyumba zao kutokana na hali ya kiusalama.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam jana na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro, baada ya jeshi hilo kubaini kuwa mauaji mengi yanayoendelea kutokea hapa nchini yanasababishwa na watu wasiofahamika ambao wamekuwa wakihama nyumba waluizopangisha mara baada ya kufanya matukio ya kihalifu.

Katika kutilia mkazo agizo hilo Kamishna Sirro amesema endapo suala hilo litapingwa na wenye nyumba jeshi hilo halitosita kuwa chukulia hatua kali za kisheria wale wote wanatakao puuzia agizio hilo la kiusalama.

Aidha, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam katika Operesheni zake imefanikiwa kukamata Pembe 20 za Ndovu huko Mbagala kwa mmoja wa askari wa jeshi la wananchi na jeshi hilo linamshikilia huyo mtuhumiwa kwa mahojiano.