Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Juma Njwayo akihutubia wakazi wa Tandahimba mjini
Akizungumza na East Africa Radio kwa njia ya simu muda mfupi baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Njwayo aliyeshika nafasi ya tatu kwa kupata kura 4,304, amesema awali alizunguka katika matawi mbalimbali na kujiridhisha kuwa aliongoza lakini katika majumuisho akajikuta ameshindwa na kuwa katika nafasi ya tatu.
Katibu wa CCM wilaya ya Tandahimba, Mohamed Manyamba, amesema mshindi katika jimbo hilo ni Shaibu Salim Likumbo aliyepata kura 4,719 akifuatiwa na Abdullah Suleiman Lutavi ambaye alipata kura 4,521 huku Juma Njwayo akiambulia nafasi ya tatu kwa kupata kura 4,304.
Hata hivyo Njwayo amekataa kusaini karatasi ya matokeo hayo kutokana na msimamo wake wa kutokubaliana nayo jambo ambalo halitoweza kubadilisha matokeo.