Kikwete amesema, bara la afrika limekuwa mwadhirika mkubwa wa mabadiliko hayo kwa kukumbwa na njaa, ukame, uhaba wa maji, kupotea kwa uoto wa asili na uzalishaji duni wa Kilimo licha ya kuwa Afrika inachangia kiasi kidogo sana cha hewa ukaa duniani.
Akiongea katika mkutano ulioandaliwa na uongozi institute jijini Dar es salaam na kuwakutanisha watunga sera, watafiti na wadau wa mazingira duniani kwa lengo la kujadili namna ambavyo dunia inavyoweza kutekeleza mkataba wa Paris juu ya mabadiliko ya tabia nchi.
"Matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi nimakubwa, waafrika wengi wamekua watu wa kuama amma, Vita kati ya wakulima na wafugaji , mafuriko na joto kali hii yote nikwasababu mazingira yamekuwa sio rafiki tena kutokana na hewa ukaa inayozalishwa tangu kuanza kwa mapinduzi ya viwanda duniani" amesema Kikwete
Kikwete amesema, nchi za bara la Afrika kwa sasa zimepiga hatu kwa kuandaa tamko la pamoja la kuikumbusha dunia nini hasa kifanyike kuhakikisha afrika inalindwa dhidi ya madhara hayo, tamko ambalo litatumika pia katika mikutano ya kimataifa ya mazingira.
Kikwete ameongeza kuwa, wakati huu ambapo Tanzania inaingia kwente uzalishaji wa viwanda nivyema tukafikiria kuwa na uzalishaji wa viwanda utakaolinda mazingira ili kulinda mazingira yetu dhidi ya madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.




