Tuesday , 7th Jun , 2016

Jeshi la polisi nchini Tanzania limepiga marufuku maandamano na mikutano yote ya hadhara kuanzia leo tarehe 07/06/2016 mpaka pale hali ya usalama itakapotengemaa.

Jeshi la polisi nchini Tanzania limepiga marufuku maandamano na mikutano yote ya hadhara kuanzia leo tarehe 07/06/2016 mpaka pale hali ya usalama itakapotengemaa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna wa polisi Operesheni na Mafunzo Nsato Mssanzya amesema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa vyama vya siasa vikitaka kufanya mikutano na maandamano na jeshi hilo kubaini kuwa mikutano hiyo inalengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi.

Aidha jeshi la polisi linawataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi hii na badala yake linawasihi waendelee kushirikiana katika kujenga umoja wa nchi.