Thursday , 20th Nov , 2014

Serikali imeitaka jamii kuisaidia serikali kuondoa tatizo la watoto wa mitaani kwa kutumia vituo vya watoto yatima na walioko kwenye mazingira magumu

Naibu Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto Mh. Pindi Chana

Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto imeitaka jamii kuisaidia serikali kuondoa tatizo la watoto wa mitaani kwa kutumia vituo vya watoto yatima na walioko kwenye mazingira magumu ili kuwaepusha na ukatili mbalimbali wanaokutana nao.

Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mh. Pindi Chana wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya kutetea haki za watoto chini ya shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Mh. Chana ameeleza kuwa serikali imeendelea na jitihada mbalimbali za kuwaepusha watoto na matatizo mengi yanayowakabili kwa kuhakikisha kuwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanapelekwa shule na kupata haki nyingine ili kuwaepusha na ukatili