Kaimu Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma
Akizungumza leo na waandishi wa habari Jijini Arusha, kuhusiana na sababu za Majaji wa Mahakama Kuu na Rufaa nchini, kukutana Jijini hapa kwa siku tano, ili kupeana mafunzo jinsi ya kuboresha utendaji kazi wao, Jaji Prof. Ibrahimu amesema mwaka 2014 walikuwa Majaji 90, mwaka jana walikuwa 75 na sasa wapo 69.
Amesema kutokana na kupungua kwa Majaji hao kunasababisha jaji mmoja kuelemewa na mzigo kwa kusikiliza mashauri 478, badala ya kuwa na jalada za kesi 178.
“Lakini hata hivyo tunajitahidi angalau wasikilize majalada zaidi ya 200, japo ni mzigo mkubwa kwetu na inahitajika tujitahidi kutatua changamoto hiyo,” alisema.
Amewataka mahakimu kusimamia misingi ya maadili yao ya kazi na kuzingatia sheria zinavyotaka, katika utoaji wa haki bila kuingiliwa au kushinikizwa na mtu yoyote.
“Watoe haki za watu bila uoga kwa kufuata maadili yao ya kiapo walichokula, ili watu wazidi kujenga iamani na mhimilia huu wa mahakama,” alisema.
Jaji. Prof. Ibrahimu alisema katika kuboresha utendaji kazi wao, wapo mbioni kuboresha Chuo cha Lushoto, Mkoano Tanga, ili kiweze kutoa mafunzo kwa Mahakimu na Majaji hasa sheria mpya zinatotokea.
“Hii ipo mbioni sababu serika kwa kushirikiana na Benki ya dunia imetoa fedha kwa ajili ya kuboresha Chuo hiki kiendane na mazingira ya utoaji mafunzo na kuwanoa watumishi wa Mahakama,” alisema.
