Tuesday , 27th Sep , 2016

Wakuu wa idara wa halmashauri na taasisi mbalimbali za serikali wameaswa kutenda haki na kuacha tabia ya kudai rushwa ili kupandisha watumishi madaraja au kutoa nafasi za kazi kwa upendeleo.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Seleman Jaffo.

Hayo yamezungumzwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jaffo, Mkoani Mara, wakati wa ziara yake ya kuongea na watumishi na wakuu wa idara katika Manispaa ya Musoma na Halmashauri ya Wilaya ya Musoma

Mhe. Jaffo amesema mara nyingi sana watumishi wengi wanakumbana na hali ya kujipendekeza au kuombwa rushwa ikiwemo rushwa ya ngono ili waweze kupandishwa madaraja hali ambayo inawanyima haki yao ya msingi ya kulitumikia taifa.

Aidha Waziri Jaffo ambaye alitembelea maeneo mbalimbali mkoani humo ikiwemo mradi wa hospitali ya rufaa inayojengwa eneo la Kangwa ambapo ametumia fursa hiyo kuwataka watumishi hao kufanya kazi kwani serikali ya awamu ya tano inawajali sana.