Monday , 22nd Jul , 2019

Msanii wa miondoko ya muziki wa Taarab na BongoFleva kwa sasa Isha Mashauzi "Jike la Simba" ametoa neno kwa wale wote wanaotumia dawa za kujibusti ili kuongeza nguvu na muda kitandani.

Isha Mashauzi amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio  Digital, baada ya kuulizwa kama mpenzi wake anatumia njia hizo akiwa kitandani na kuhusu vijana ambao wanatumia dawa hizo.

"Sipendi kusalitiwa, na mpenzi wangu wa zamani aliwahi nisaliti sio kwa sasa hivi na siwezagi kuzungumzia vitu kwa undani zaidi yaani hapo "No Comment" , Wajibusti tuu kila mtu afanye kitu ambacho yeye anajiskia kufanya ili mradi kisiwe na madhara mbeleni kwenye maisha yake au maisha ya mtu mwingine. Ila kama mtu anafanya afanye hakatazwi". amefunguka.

Aidha msanii huyo kwa sasa amesema anahamia kwenye game ya BongoFleva kwa muda kwa sababu ni muziki ambao unapendwa na watu wengi zaidi, ndio maana anaendelea kuufanya kama alivyowaonjesha kwenye wimbo wa "Nimpe nani" wenye ladha ya BongoFleva, lakini amesisitiza hawezi kuucha muziki