Vikosi vya uokoaji vinaendelea na zoezi la kuwatafuta watu waliokwama katika vifusi vya jengo hilo kufuatia tetemeko hilo lililotokea jana, ambapo tarifa za awali zinasema watu kadhaa waliojeruhiwa katika ajali ya jengo hilo wamelazwa katika hospitali mbalimbali katika mji huo.
Rais wa nchi hiyo Ma Ying-jeou ameahidi kuimarisha vikosi vya uokoaji baada ya kuwasili katika mji huo kusimamia juhudi za uokoaji watu waliokwama katika vifusi vya jengo hilo ambalo lilikuwa ni makazi ya watu.



