Monday , 23rd Jun , 2014

Benki ya dunia ofisi ya Tanzania kesho inazindua ripoti ya hali ya uchumi nchini ambapo waziri mkuu Mizengo Pinda atakuwa mgeni rasmi.

Waziri mkuu wa Tanzania mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda.

Taarifa iliyotolewa na afisa mawasiliano wa benki hiyo Bi. Loy Nabeta imesema kuwa ripoti hiyo inatolewa wakati ambapo takribani watu milioni moja hutafuta ajira nchini Tanzania kila mwaka.

Kwa mujibu wa Nabeta, idadi kubwa ya wanaotafuta ajira hukimbilia maeneo ya mijini ambako wanadhani ndiko kwenye ajira na maisha mazuri, huku takwimu zikionyesha kuwa takribani watu milioni 15 huishi mijini.