Wednesday , 12th Nov , 2014

Mkoa wa Geita unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mauaji ya akinamama vikongwe yanayotokana na imani za kishirikina na migogoro ya kifamilia ambayo inahitaji kupatiwa ufumbuzi ili kuimarisha ustawi wa jamii.

Akiongea wakati wa makabidhiano ya mkoa wa Geita, aleiyekuwa Mkuu wa mkoa huo ambae sasa anahamia mkoa wa Lindi, Magalula S. Magalula amesema serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imesaidia kuzitatua changamoto hizo na kuhakikisha kuwa wale wanaojihusisha na mauaji hayo wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa mpya wa Geita ambae amehashiwa hapo akitokea mkoani Tabora, Fatuma Mwasa amesema anapokea kijiti cha uongozi wa mkoa huo na atahakikisha mipango ya maendeleo iliyoanzishwa inaendelezwa na ametaka wananchi kutoa ushirikiano katika kutatua changamoto za kimaendeleo zinazoukabili mkoa huo.

Wanawake wengi wazee katika Mkoa huo wanasadikiwa kuuawa tangu mwaka 2010 kutokana na kuhisiwa kuwa ni washirikina huku vikongwe wengine wakiwa mashakani kutokana na matukio hayo.