Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),George Simbachawene
Hayo yamesemwa leo na Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),George Simbachawene wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa elimu bure mjini Dodoma.
Amesema fedha hizo zitatumika katika kugharimikia masuala mbalimbali ya elimu ikiwemo ruzuku ya uendeshaji wa shule, chakula cha wanafunzi wanaokaa bweni, fidia ya ada ya shule za sekondari za kutwa sh. Elfu 20 na bweni sh elfu 70 pamoja na gharama za mitihani ya kidato cha nne ambapo wazazi na walezi
Aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri husika kuhakikisha fedha hizo zinafika kwa wakati na zinatumika kwa kazi iliyokusudiwa.
Simbachawene alisema majukumu ya wazazi pamoja na mambo mengine yatakuwa ni kununua sare za shule, vifaa vya kujifunzia, gharama za matibabu, nauli, gharama za chakula kwa wanafunzi wa shule za kutwa na kununua magodoro, shuka, vifaa vya usafi binafsi kwa wanafunzi wa bweni.