
Dkt. Kijaji amesema hayo leo bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mtambile Masoud Abdallah Salim (CUF), aliyehoji mkakati wa Serikali wa kufanyia tathmini deni hilo.
Katika swali jingine, Salim amesema deni la taifa linaongezeka na serikali inaendelea kukopa kwa masharti ya kibiashara yanayoisababishia nchi hasara, kwamba kwa sasa Serikali inataka kukopa shilingi trilioni nne, kuhoji kama serikali itaweza kulipa kulingana na hali ya uchumi ya sasa.
Katika majibu yake Dkt. Kijaji amesema, “Serikali haijawahi kuacha kulipa katika taasisi yoyote ndiyo maana tunaendelea kuaminika na tutaendelea kukopa kwa uangalifu mkubwa na tunapokopa tunaelekeza fedha katika maeneo yenye tija.