Tuesday , 4th Apr , 2017

Mkuu wa wilaya ya Mtwara Evodi Mmanda ametoa muda wa siku Saba kwa uongozi wa Kitongoji cha Mkaya, kilichopo kata ya Naumbu kuhakikisha wakazi wake wanahama na kutafuta sehemu nyingine za kuishi

Evod Mmanda

Sababu ya maamuzi hayo ni kutokana na eneo hilo kutokuwa makazi rasmi ya kuishi pamoja na kukosa kuwa na huduma za kijamii.

Agizo hilo amelitoa baada ya kufika katika kitongoji hicho, ambacho kipo pembezoni mwa Bahari ya Indi akiwa na kamati yake ya ulinzi na usalama, ambapo wananchi wake huishi katika nyumba za Makuti huku shughuli zao kuu zikiwa ni Uvuvi haramu.

Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Juma Salum, amekiri kulipokea agizo la mkuu wa wilaya na kuahidi kulitekeleza huku baadhi ya wakazi wa kitongoji hicho akiwamo Hassan Mfaume akitii agizo.

Mkuu huyo wa wilaya amesema atarudi tena katika kitongoji hicho Aprili 9 kwa ajili ya kuangalia utekelezaji wa agizo lake.

Sikiliza 

Sauti ya DC Mmanda
Sauti ya Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Juma Salum na mkazi Hassan Mfaume