Sunday , 29th Nov , 2015

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam Dkt. Aziz Msuya amesema ili ugonjwa wa kipindupindu uweze kumalizika ni lazima wakazi wa jiji waache tabia ya kujiunganishia maji

hovyo kutokana na wengi waliogua wametokana na kunywa maji yasiyo chemshwa na yenye kinyesi.

Akizungumza na East Africa Radio leo juu ya hali ya ugonjwa wa kipindupindu katika Manispaa ya Kinondoni Dkt. Msuya amesema hadi kufikia leo kambi ya wagonjwa hao ya Mburahati ilikuwa na wagonjwa wanne tu huku kambi ya wagonjwa hao ya Mwananyamala ikiwa haina mgonjwa hata mmoja.

Ameongeza kuwa hali ya mazingira na miundombinu ya Dar es salaam hairidhirishi na hivyo kuwataka wananchi kuchukua tahadhari kubwa kwa kutoa taarifa kwa wataalam wa afya.