Monday , 11th Mar , 2019

Kufuatia ajali ya ndege aina ya Boeing 737 ya Shirika la Ndege la Ethiopia iliyokuwa ikitoka Addis Ababa kwenda Nairobi kuanguka na kuua watu 157, Mamlaka ya Udhibiti wa Safari za Anga ya nchini China imeingilia suala hilo.

Boeng 737 mali ya Shirika la Ndege la China

Mamlaka hiyo imesema mapema Jumatatu, Februari 11 kuwa imeliagiza Shirika la Ndege la China kusitisha matumizi ya ndege za Boeing 737 hadi hapo itakapotoa taarifa zaidi kuhusu kurejea kwa safari zake.

Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia aina ya 737 MAX 8 ilipata ajali dakika chache baada ya kuruka katika Uwanja wa Ndege wa Addis Ababa Jumapili, Februari 10. 

Hiyo ni ajali ya pili ya ndege hizo ambazo ni toleo jipya la kampuni ya Boeing lililotolewa mwaka 2017, ambapo mnamo Oktoba mwaka 2018, ndege ya Shirika la Ndege la Indonesia iliyokuwa ikifanya safari za ndani ilianguka dakika 13 baada ya kuruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Jarkata na kuua abiria 189 pamoja na wahudumu wa ndege.

Shirika la Ndege la China linamiliki jumla ya ndege 96 aina ya Boeng 737 MAX, ambapo imesema imeona mfululizo wa vyanzo vya ajali za ndege hizo zinafanana.

Lakini msemaji wa Shirika la Ndege la Boeing ameuambia mtandao wa Reuters akikanusha tuhuma hizo za China, akisema kuwa hana uhakika na taarifa ambazo nchi hiyo inazitumia.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali za kimataifa, mpaka sasa zaidi ya mataifa takribani sita yamesitisha matumizi ya aina hiyo ya ndege kwa kuhofia usalama wake. Mataifa hayo ni pamoja na China, Korea Kusini, Ethiopia, India na Uingereza, ambapo nchi za Uingereza na India zimepiga marufuku ndege hizo kupita juu ya anga zake.

Bonyeza hapa chini kutazama Zaidi.