
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo
Ndikilo ameyasema hayo katika kikao cha kawaida kati yake na watendaji wa mkoa wake ambapo amebainisha kuwa jumla ya kaya 8449 zinahitaji chakula kiasi cha tani 440 ili kuweza kunusuru hali iliyopo kwa sasa.
“Hali ya chakula katika Halmashauri ya Chalinze siyo nzuri hivyo kuna upungufu wa tani 440 jambo ambalo linahitaji usaidizi wa haraka ili kuokoa maisha ya wananchi ambao wanakabiliwa na ukosefu wa chakula” Amesema Ndikilo.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema tayari mkoa wake umefanya mawasiliano na Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha maafa ili kuweza kupata msaada wa dharura.