Wednesday , 4th Jul , 2018

Mbunge wa Iringa Mjini, Mch. Peter Msigwa ametia nadhiri ya kwamba uchaguzi ujao wa mwaka 2020 anaamini chama chake kitakwenda kushinda kwa kishindo kikubwa kwa sababu serikali iliyopo madarakani imeshindwa kufanya kazi na kutimiza yale waliyoahidi wakati wa Uchaguzi mkuu 2015.

Mbunge wa Iringa Mjini, Mch. Peter Msigwa.

Mch. Msigwa ameyasema hayo leo wakati akizungumza na www. eatv.tv kuhusiana na namna CHADEMA ilivyojiandaa na ushindani wa mwaka 2020 katika uchaguzi mkuu.

Msigwa amesema kwamba, wananchi wameona ni kwa kisi gani walivyodanganywa na namna ahadi nyingi zilizotolewa zimeshindwa kutekelezwa hivyo anaamini kwamba hawataweza kufanya kosa la kuirudisha CCM madarakani.

"Ushindi wa Chadema 2020 utakuwa ni wa kishindo sana. Wnanchi wamejionea namna ambavyo Rais ba seriikali yake walivyoshindwa. Kila mahali wananchi wanalia, Rais hataki kukosolewa, hataki kuwapa nafasi watu wengine ya kuzungumza. Ameshindwa kazi aliyopewa na wananchi na uhakika ushindi wetu utakuwa ni wa Kimbunga," Msigwa.

Akizungumzia kuhusu suala la yeye kufikiria kuwa Rais siku moja kupitia chama chake, msigwa amesema bado hajapata maono hayo.

"Urais mimi bado sijawahi kuufikiria. Mimi nadhani zaidi nahitaji kuwatumikia wananchi kwa ngazi ya Ubunge lakini urais hapana. Lakini ushindi wetu wa 2020, tunaamini unaanzia kwenye ngazi ya urais mpaka kwenye Kata".