Friday , 21st Sep , 2018

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeitaka serikali kuweka utaratibu wa kuwafidia marehemu pamoja na majeruhi wa ajali ya Mv-Nyrere iliyotokea mapema jana.

Kupitia Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Freeman Mbowe amesema tukio hilo ni msiba wa kitaifa wenye majonzi huku akiitaka serikali kundaa utaratibu utakaowafariji waathirika wa ajali.

Tunaitaka serikali ijiandae kulipa compassion (fidia) kwa watu waliopoteza maisha yao, katika kivuko cha kile, ni utaratibu wa kawaida kwa vyombo vya usafiri lazima vikatiwe bima, ili familia zilizoathirika ziweze kujifuta machozi, ”

Katika hatua nyingine Chadema imependekeza uwajibikaji kwa viongozi wa taasisi husika kwa kile walichokidai ubovu wa kivuko hicho kilisharipotiwa na Mbunge wa Jimbo la Ukerewe Joseph Mkundi.

Watu wawajibike kwenye uzembe huu, kama angewajibika waziri, katibu mkuu waziri atakayeingia atakuwa na tahadhari, tunamtaka Rais achukue hatua awawajibishe, amewajibisha watu wengi kwa makosa ya ufisadi, tunamtaka hili, lazima tufike tuliowapa mamlaka wachukuliwe hatua.

Shughuli za ukoaji wa miili bado linaendelea kufanywa na vyombo vya ulinzi na usalama. Hadi sasa miili ya watu 125 tayari imeopolewa katika zoezi la uokoaji linaloendelea.