Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt Vincent Mashinji amesema awali walionekana kutii agizo hilo la katazo ya mikutano ya kisiasa kwa sababu chama hicho kilikuwa kinashughulika na ujenzi wa chama chake.
Mashinji amesema, "ni kweli tulikuwa na jukumu la ujenzi wa chama kama taasisi, kwa hiyo tulikuwa hatuna uwezo wa kuendesha vitu viwili kwa wakati mmoja."
"Ndiyo maana wakati tamko linatokea na matendo yetu ilionekana kutii amri isiyokuwa halali bali ni matukio mawili ambayo yaliyotokea kwa wakati mmoja na moja kumeza jingine." ameongeza Mashinji.
Kuhusiana na Uchaguzi wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Katibu Mkuu huyo amesema kupitia kamati kuu wameandaa mikakati ambayo itawafanya kuibuka na ushindi.
Akipokea ripoti ya Tume ya Taifa Uchaguzi NEC, June 07, 2016 Rais Magufuli aliwataka viongozi wa kufanya siasa hadi 2020, lakini kwa sasa wawape nafasi viongozi waliochaguliwa kutekeleza waliyoyaahidi.