Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Ndg. Vuai Ali Vuai
Akizungumza kuhusu mwenendo wa kampeni visiwani humo Naibu Katibu mkuu wa Chama hicho Visiwani Zanzibar Bw. Vuai Ally Vuai amesema kuwa chama hicho hakina wasiwasi na utaratibu huo kwa kuwa kina uhakika wa ushindi.
Ameongeza kuwa pia utaratibu huo utakisaidia chama hicho pia kujua idadi ya kura walizozipatas katika ngome ya Wapinzani viwasani pemba ambayo itawajenga na kukiimarisha zaidi chama hicho.
Vuai ameongeza kuwa chama chake kimeiridhisha kushinda katika uchaguzi mkuu mwaka huu kuanzia ngazi ya madiwani hadi urais kwa sababu wananchi wameonesha kuwa na imani na chama hicho kwa kuwa kimetekeleza sehemu kubwa ya ahadi za mwaka 2010.