Katibu wa Idara ya Uenezi Afisi Kuu Zanzibar Ndg Waride Bakari Jabu akiwahutubia Wananchi
Akizunguza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya chama hicho visiwani humo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Zanzibar Bi. Waride Bakari Jabu amesema kamati maalumu imewataka wanachama wake kujiimarisha na kujiweka tayari kwa ajili ya uchaguzi wa marudio.
Waride amesema kuwa baada ya Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu hakuna mgombea yoyote ambaye anaweza kuapishwa kuwa Rais wa Zanzibar kupitia matokeo ya uchaguzi huo.
Wakati CCM, na CUF wakiendelea kujadiliana chama cha ADA-TADEA kupitia mkurugenzi wake wa habari, Rashid Mchenga kimesisitiza umuhimu wa kufuata katiba huku kikishangazwa na majadilano hayo kuwa ni ya vyama viwili tu wakati uchaguzi ulikuwa na vyama 14.