Wataalamu wa Mashine za BVR, wakizikagua mashine hizo kabla hazijapelekwa vituoni.
Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura limeanza rasmi leo Jijini Dar es Salaam kwa muitikio mkubwa wa wananchi kujitokeza huku changamoto mbalimbali zikijitokeza ikiwemo kuchelewa kwa kuanza Uandikishaji huo.
East Africa Radio imepita katika vituo mbalimbali vya uandikishaji na kushuhudia baadhi ya vituo vikiwa na changamoto ya ubovu wa mashine na kufanya watu kukaa muda mrefu bila kujiandikisha huku baadhi ya vituo, maeneo ya Tabata, Kiwalani, Karakata, Makumbusho vituo vimechelewa kufunguliwa katika muda uliopangwa.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa uchaguzi wa NEC, Julius Malaba amesema mashine zilizoagizwa kwa ajili ya uandikishaji nchi nzima ni elfu nane na zinazotarajiwa kutumiwa kwa Dar es Salaam ni 3000 tu.
Aidha malaba ameongeza kuwa mashine kila kituo kitakuwa na BVR kits mbili lakini vituo vitaongezewa mashine hizo kutokana na wingi wa watu watakaojitokeza kujiandikisha.