Thursday , 9th Jul , 2015

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha Mswada wa Sheria ya Kuundwa kwa tume ya utumishi wa Umma licha ya akidi ya upitishwaji wa Miswada Bungeni kutotimia.

Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Anne Makinda akitoa taarifa kwa Wabunge.

Muswada huo ambao umepitishwa huku baadhi ya marekebisho yaliyotolewa na kamati ya kudumu ya Bunge huduma za jamii chini ya Mwenyekiti wake Bi. Magret Sitta kukataliwa.

Kabla ya kupitishwa kwa muswada huo Mbunge wa Nzega, Dkt. Khamis Kigwangala alisimama kutoa taarifa kwa spika na kusema kuwa uamuzi wa kupitishwa kwa muswada huo ni batili kutokana na akidi kutotimia.

Licha ya Taarifa ya kutotimia akidi na Mbunge huyo kuomba Spika aweze kuhesabia wabunge waliomo, Spika Bi. Anne Makinda alikataa taarifa hiyo na kusema sio wakati wake na hakuwa na hoja hivyo kuwahoji wabunge na wote kukubali kupitshwa kwa muswada huo.