Picha ya jiji la Dodoma
Muswada huo umefikishwa katika bunge la kumi na mbili na kikao cha kwanza la Jamhuri ya muungano wa Tanzania jijini Dodoma, ambalo litakaa kwa wiki mbili likiwa na mahususi kwa ajili ya uwasilishwaji wa miswada ya sheria.
Akiwasilisha maelezo ya serikali kuhusu muswada huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, Seleman Jafo amesema kuwa chimbuko la hoja ya kutunga sheria hiyo ni kutokana na kukosekana kwa sheria inayotambua na kuweka misingi ya uendelezaji wa makao makuu ya nchi na kukosekana kwa kutofikia malengo ya uendelezaji wa makao makuu ya nchi.
Baada ya wabunge kujadili mswada huo na kuupitisha bunge litaendelea kujadili na kupitisha miswada mingine itakayowasilishwa bungeni na serikali katika kipindi chote cha bunge la 12.
Kupitisha kwa muswada huo kutafanya wazo lolote la kubadilisha makao makuu ya nchi kuhitaji theluthi mbili ya wabunge wote wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kukubali wazo hilo.