Wednesday , 30th Nov , 2016

Bunge la Senate nchini Colombia limeidhinisha mapendekezo ya kuleta amani yaliyofanyiwa mapitio kwa pamoja na  kundi kubwa la waasi la Farc.

Bunge la Seneti nchini Colombia

 

Makubaliano ya awali yalikataliwa kwa kura chache katika kura ya maoni iliyopigwa mwezi uliopita.

Rais wa nchi hiyo Juan Manuel Santos amesema mapendekezo mapya yana nguvu na yakizingatia madai ya mabadiliko yaliyotolewa na wapinzani.

Hata hivyo upande wa upinzani unaoongozwa na Rais wa zamani wa nchi hiyo  Alvaro Uribe, amesema mapendekezo hayo yaliyofanyiwa mapitio bado hayakidhi matakwa ya viongozi wa FARC. mapendekezo hayo yanapelekwa bunge la chini kwa ajili ya kuidhinishwa.