Tuesday , 9th Feb , 2016

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Lazaro Mambosasa amesema wamefanikiwa kuikamata bunduki iliyotumika kuitungua helikopta na kumuua rubani wake Rodgers Gower (37) raia wa Uingereza katika tukio lililotokea ndani ya pori la akiba wilayani Maswa

Bunduki hiyo aina ya Riffle Na 7209460 CAR Na 63229, imepatikana mara baada ya jeshi la polisi kufanikiwa kuwakamata watu 9 wanaotuhumiwa kuhusika na tukio hilo.

Kamanda Lazaro Mambosasa amesema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na jeshi hilo kushirikiana na wananchi, pamoja na uongozi wa TANAPA.

Aidha waliokamatwa wamekiri kuhusika na tukio hilo, huku akieleza kuwa msako mkubwa ulifanywa na jeshi hilo mara baada ya tukio kutokea chini ya mkuu wa upelelezi mkoa Jonathan Shana.