Thursday , 7th Jan , 2016

Mamlaka ya maji ya mji mdogo wa Ngaramtoni Jijini Arusha imewataka wananchi waliojenga kwenye vyanzo vya maji kubomoa nyumba hizo kwa muda wa siku 90 ikiwa ni utekelezaji wa sheria ya mazingira

Meneja wa Mamlaka ya maji mji mdogo wa Ngaramtoni Clayson Kimaro

Wakizungumza katika zoezi la kuweka alama nyumba hizo zilizojengwa katika chanzo cha maji cha Sailoja kilichopo kata ya Kiranyi ,Wananchi hao ambao ni wahanga wa zoezi hilo wameiomba serikali iwapatie maeneo mbadala licha ya kuyamiliki maeneo hayo kihalali na kulalamikia kuwa bomoa bomoa hiyo huenda ikarudisha nyuma maendeleo ya wananchi.

Diwani wa Kata ya Kerai John Edward amezitaka mamlaka husika zinazotekeleza sheria hiyo kufanya mazungumzo na maridhiano na wananchi ili kuepuka migongano inayOweza kutokea baina ya wananchi na serikali.

Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya maji mji mdogo wa Ngaramtoni Clayson Kimaro amesema kuwa zoezi hilo limezingatia sheria ya maji na litasaidia upatikanaji endelevu wa maji hivyo amewataka wananchi wapishe vyanzo vya maji .

Ombwe la wananchi na taasisi za taasisi serikali kujenga katika vyanzo vya maji ni tatizo sugu nchini linalohitaji tiba ya kisheria ili kuepuka athari za uhaba wa maji zinazojitokeza na zitakazojitokeza miaka ya baadae.