Wednesday , 17th Feb , 2016

Serikali nchini Burundi imepiga marufuku matumizi ya usafiri wa pikipiki kuingia katikati mwa mji mkuu Bujumbura katika juhudi za kujaribu kupunguza mashambulio yaliyojitokeza katika mji huo.

Jeshi la Polisi wamegundua kwamba wahalifu hubeba mabomu wakitumia mabegi au vikapu,” Bw Mbonimpa anasema.

Usalama umeimarishwa mjini humo tangu kutokea kwa mashambulio hayo na polisi wanapekua watu na magari ili kuhakikisha hali kama hiyo inadhibitiwa.

Aidha machafuko yalizuka nchini Burundi Aprili mwaka jana Rais Pierre Nkurunziza, ambaye amekuwa uongozini tangu 2005, alipotangaza kwamba angewania urais kwa muhula wa tatu.

Hadi sasa watu 400 wamefariki na wengine 240,000 kutorokea nchi jirani kutafuta malazi na makazi.