Wednesday , 26th Oct , 2016

Serikali imeombwa kutoa shilingi bilioni moja kwa ajili ya kukarabati vituo vya afya vinavyotoa huduma ya uzazi kwa mama na mtoto nchini.

Akina mama wajawazito katika harakati za uzazi

 

Ombi hilo limetolewa na Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama Bi. Rozi Mlay wakati akizungumza na wadau wa afya kutoka sehemu mbalimbali, waliokutana kwa ajili ya kuweza kupanga namna ambavyo wataweza kuhamasisha serikali na wananchi kwa pamoja waweze kutoa kipaumbele ili mwanamke anapoenda kijifungua awe salama kiafya yeye na mtoto wake.

Kwa upande wake Mtaalamu wa Masuala ya Uzazi nchini Stellah Masala Mpanda ameitaka serikali iweke vifaa maalum kwa ajili ya wakina mama hao vya kujifungulia na kuacha kuwaagamiza kina mama wajawazito vifaa kutoka majumbani mwao kwakuwa vingine wanavyobeba havina usalama kiafya.