Wednesday , 3rd Feb , 2016

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imeshusha bei ya mafuta ya aina ya dizeli kwa shilingi 1600 kwa mkoa wa Dar es salaam kutoka shilingi 1747 ikiwa ni shilingi 147 chini.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngalamgosi

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi amesema kushuka kwa bei hizo kunatokana na kuendelea kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na gharama za uasafirishaji nchini.

Bidhaa zingine za mafuta Petroli imeshuka kwa shilingi 55 na kufanya mafuta hayo kuuza kwa shilingi 1,842 kutoka 1997 tangu mwezi uliopita.

Ngamlagosi ameongeza kuwa EWURA inavikumbusha vituo vyote vya mafuta kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.

Aidha EWURA inawashawishi wanunuzi kuhakikisha wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo,tarehe aina ya mafuta yanayonunulia kwa lita.