Wednesday , 13th Jul , 2016

Lengo la Mamlaka ya Bandari ya Tanzania kukusanya shilingi Trilioni 1 kwa mwaka kutoka Bilion 6 za sasa linaweza kufanikiwa kama watendaji na watumiaji wa bandari hiyo watakuwa wazi katika utekelezaji wa majukumu yao na kuacha udanganyifu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA Mhandisi Deusdedit Kakoko, alipokuwa akifafanua kuhusu taratibu zinazochukuliwa na bandari hiyo ili kuhakikisha inakuwa na ushindani na bandari nyingine duniani.

Amesema mamlaka hiyo imeanza kubadilisha mifumo mbalimbali hasa ile ya TEHAMA ambayo ilikuwa inachangia sana upotevu wa mizigo ya wateja bandarini pia kubadilisha muundo mpya wa ufanyaji kazi katika bandari hiyo.