Thursday , 14th Jan , 2016

Halmashauri ya Bagamoyo Mkoani Pwani inaongoza nchi nzima kwa udanganyifu wa uuzwaji wa ardhi kwa watu binafsi,kughushi Mihutasari ya majina pamoja na kutumia ardhi kukopea mabilioni ya fedha kwa maslahi binafsi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi

Akizungumza na Watendaji wilayani Bagamoyo katika ziara yake ya kikazi waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema kuwa kuanzia sasa utaratibu wa uuzwaji wa ardhi ubadilishwe na kuwashirikisha wakuu wa wilaya.

Mhe.Lukuvi ameongeza kuwa Wilaya hiyo inaongoza kwa kughushi kutokana na kuwa na mikutano mingi feki ikiwa ni pamoja na watu kuuziana Ardhi jijini Dar es Salaam na kupelekea vivuli tu za mikataba ambayo haijakidhi viwango vya uuzwaji.

Akiwa wilayani humo Mhe.Lukuvi alitembelea masijara ya ardhi na kuvumbua madudu ikiwemo ucheweleshwaji wa hati za viwanja kwa watu wasiokuwa na kipato huku matajiri wakiharakishiwa huduma hiyo huku baadhi ya watendaji wakishindwa kutimiza wajibu wao.