Saturday , 26th Sep , 2015

Askofu mkuu wa kanisa katoliki jimbo kuu la Dar es salaam Kardinali Polycarp Pengo amewataka watanzania kuhakikisha siasa na harakati za uchaguzi haziwatengi na kuwagawanya kimakundi na kuondoa amani baada uchaguzi.

Askofu mkuu wa kanisa katoliki jimbo kuu la Dar es salaam Kardinali Polycarp Pengo

Askofu Pengo ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akiongea na East Africa Radio juu ya maoni yake kama kiongozi wa kanisa katoliki Dar es salaam moja ya makanisa yenye waumini wengi na kubwa duniani.

Katika hatua nyingine Kardinali Pengo ameitaka serikali isiruhusu siasa isiingilie suala la elimu kwani elimu ni msingi mkubwa wa kizazi cha sasa kinachokabiliwa na changamoto ya kuongezeka kwa maarifa.

Askofu Pengo ametoa rai hiyo mara baada ya kuzindua shule ya chekechea ya Santa Rita iliyojengwa na wahisani kutoka Italia na Sherehe zilizohudhuriwa na Balozi wa Italia hapa nchini Luigi Scotto ambaye pia ameendelea kusisitiza umuhimu wa elimu.