IGP Ernest Mangu
Taarifa kutoka wilayani Kibiti mkoani Pwani zinadai kuwa askari hao wameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi wakati wakijiandaa kuondoka kwenye lindo ili warudi kituoni.
Chanzo cha kuaminika kutoka eneo la tukio kimesema "Magaidi walimshambulia dereva wa gari ya askari kwa risasi na gari likapunduka, wakawamiminia askari wote risasi mpaka sasa kuna mili 6 ya askari iliyopatikana"
Pia kuna tetesi kuwa silaha zote (SMG) zimeibiwa.
Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, hawakuwa tayari kuzungumzia tukio hilo, huku simu za Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania , Mkuu wa Mkoa wa Pwani pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani, zikiita bila majibu.



