
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Juni 6 mwaka huu kwa kumpiga kwa mtwangio [mwichi] kichwani na kufa papo hapo na kisha kutoroka na siku iliyofuata akapatikana akining'inia juu ya mti amejinyonga kwa shuka.
Kamanda Mponjoli Rodson amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kukemea pamoja na kuitahadharisha jamii kuhusiana na matukio ya aina hiyo.
Amesema chanzo cha mtuhumiwa kujinyonga baada ya kumuua mkewe kunadaiwa ni mkewe kumtuhumu kuwa amekuwa akijihusisha na vitendo vya uhalifu kauli inayodaiwa kumuudhi mtuhumiwa.
Msikilize hapa Kamanda Mponjoli Rodson akifafanua zaidi:-