Naibu Waziri wa Elimu, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Enjinia Stella Manyanya,
Akizungumza leo Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu, Naibu Waziri wa Elimu, Teknolojia na mafunzo ya Ufundi Enjinia Stella Manyanya, amesema kuwa kumekua na ada tofauti katika shule binafsi ambazo nyingine haziendani na uhalisia wa uwekezaji walioufanya.
Injia Manyanya amesema kuwa serikali imeamua kushirikisha wadau wa elimu ili kupata bei ambayo haitaathiri utoaji wa huduma lakini wakati huohuo kuwawezesha wananchi wengi zaidi kufaidika na sera ya serikali.
Aidha Injia Manyanya ametolea ufafanuzi juu ya tozo zinazotolewa na shule binafsi na kusema kuwa zinaendana na uhalisia wa utoaji wa huduma na kusisitiza wamiliki wa shule hizo waweke maslahi ya taifa mbele na sio biashara.
Aidha Naibu Waziri huyo amesema kuwa pamoja na kufanya hivyo lakini pia serikali inafanya jitihada ya kuboresha shule zake ili zitoe elimu bora huku akitoa shukrani kwa bunge kwa mchango wake wa madawati kwa shule za msingi.
Kwa upande wake Mbunge wa Songwe Mjini Mhe. Philip Mulogo,alihoji ni lini serikali itaka kwa mara nyingine na wadau wa elimu ili kufikia muafaka wa suala hilo kutokana n a umuhimu wake kwa taifa.
Akitolea ufafanuzi wa ziada juu ya suala hilo Naibu waziri wa TAMISEMA,Mhe. Selemani Jaffo amesema kuwa lengo la kuwashirikisha wadau wa sekta binafsi kwa suala hilo la utoaji elimu kuweza kuhakikisha kila mtanzania anakua na nafasi ya kupata elimu lakini pia ni kukuza sekta binafsi zinazohusika na masuala ya Elimu.